Nakumbusha!
Nauliza tu
• Inakugharim kiasi gani kumsalimia mlinzi anaekufungulia geti ukiingia kazini?
•Inakugharim kiasi gani kumuomba mfanya usafi akuruhusu upite kuliko kukanyaga mahali alipodeki na hapajakauka bado?
•Inakugharim kiasi gani kumsalimia mtu ambae mmekaa nae seat moja safarini?
•Inakugharim kiasi gani kusema Asante kama MTU amekutendea vyema??
•Wanaume Inakugharim kiasi gani Kusema samahani kwa mke wako unapokosea au unapochelewa kurudi nyumbani?
•Je Inakugharim kiasi gani kumpakulia mke wako chakula baada ya yeye kupika?
•Inakugharim kiasi gani kupokea sim na kumwambia mtu Niko ktk mazingira yasiyo rafiki kwa mawasiliano kuliko kuacha sim inaita unaiangalia tu au unakata?
•Inakugharim kiasi gani kumsalimia na kumtendea vyema mtu usiemjua?
•inakughrim nini kutoa nguo ambazo huzivai na kuwapatia wahitaji, au chakula ambacho kimebaki kuliko kumwaga kwann usiwape watu wale?
•Inakugharim kiasi gani kupokea sim ya MTU anaekudai na umwambie hujapata pesa yake bado na ukipata utampatia badala yake unazima sim, unabadilisha lain, au unakata sim yake??
•Inakugharim kiasi gani kutenda wema hata kwa yule anaekuchukia???
•kwani inakugharim kiasi gani kumnunulia nguo nzuri house girl/boy wako kukaa pamoja kula pamoja kwann yeye anakula jikoni ninyi mezani? mkitoka outing familia yako na house girl wako, basi mavazi yake na mwonekano wake tu humtambulisha, kwanini?
Ooh Mungu Yehova, wewe uliemwema kwa wingi wa neema yako utufundishe kutenda wema daima! Tuwe kama wewe ulivyo maana wewe ni Baba yetu na sisi ni watoto wako!
Amen
Bwana akubariki na kukuangazia Nuru ya uso wake, mikononi mwake akutunze daima uwe mwema!

No comments:
Post a Comment