Wednesday, 7 June 2017
Muhimu sana kwa kila mwanaume
Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wanaume wakisema wanawake wasomi na wenye vyeo ni "wasumbufu". Wengine wamefika mahala wanalishana sumu za kukwepa kuwaoa wasomi ama wenye vyeo.
Kuna mambo ya kufahamu hapa. Mosi, hakuna mwanamke mkorofi mbele ya mwanaume mwenye kutumia "akili". Hata kama mwanaume ukiwa darasa la saba "B" na mwanamke akawa "Profesa", ukiishi nae kwa akili atakuheshimu na ndoa itakuwa na amani. Tatizo ni kwamba wanaume wengi wanataka kuishi na wake zao kwa "ubabe na utemi".
Kwamba wewe (mwanaume) ujiachie na wanawake wengine (upendavyo), na mke akilijua hilo hutaki kuulizwa wala kuguswa, lakini yeye(mkeo) ukimuhisi tu (kuhusiana na wanaume wengine) bila hata ushahidi unawaka hadi kwa washenga! Kwamba badala ya kumshawishi kwa "akili na upendo" katika mambo ya familia, unataka zile za "Nimesema", "Mimi ndio mwanaume humu ndani", "Ole wako ushike simu yangu" mara sijui "Nimeshaamua sitaki mjadala". n.k.
Kama unataka "stress" nenda na wanawake wa "kidijitali" kwa mtindo huu. Jambo la kuelewa ni kwamba "zama zimebadilika", hakuna mwanamke alie tayari kupelekeshwa hata kama hajasoma. Wanawake ni viumzenuazuri sana, usiwapake matope kwa ukosefu wako wa "akili" za kuishi nao. Mwanamke yeyote (msomi ama asiesoma) mbele ya mwanaume "mwenye akili" ni kama boflo ndani ya chai.
La pili ni kwamba, mtu anaekimbilia kuoa wanawake wasiosoma (akiwaogopa waliosoma ama wenye mafanikio) ni kwamba hajiamini na anachokitafuta ni kumpata mwanamke wa kumuonea kirahisi, maana anajua hakuna "msomi" ataruhusu huo upuuzi. Uhalisia ni kwamba, mwanaume asiejiamini hafai katika ndoa iwe kwa kuoa msomi ama asiesoma. Ninajiridhisha kwamba ndoa nyingi zinasumbua siku hizi sio kwa sababu wanawake wa siku hizi wamekua wakorofi, la hasha! Isipokuwa ni kwa sababu wanaume wengi wameshindwa kujiongeza "kiakili", ili zitoshe kumudu mabadiliko yanayotokea kwa kasi katika jamii ya wanawake.
Unachotakiwa kujua ni kwamba huenda ameshakusoma na kugundua eidha una akili isiyojielewa na ubabe wa kijinga, ama una zile elements za kubweteka na kutaka kulelewa kupitia efforts zake! Kwa asili ni kwamba wanawake WOTE wanafurahi kuongozwa na kukabidhi KILA WALICHONACHO kwa wanaume wenye akili na wanaojua sayansi ya kupenda. Bahati mbaya ni kwamba huwezi kumlazimisha mwanamke akutii "from no where". Mwanamke anamtii mwanaume mwenye vifaa viwili AKILI na UPENDO. Kingine cha kujua ni kwamba wanawake wa kidijitali (wa zama hizi) huwezi kuwakomoa na ukijaribu kufanya hivyo, wanaweza kujibu mapigo na mwishoni mwanaume ndio ukaonekana "bwege".
Ole wa wanaume mnaowaweka wake zenu (wenzi wenu) njia panda! Mifukoni hamueleweki, kwenye matunzo ya familia hamjali na vitandani mnaparua kama kuku. Mnawatesa hawa viumbe, jueni kwa hakika ya kwamba, machozi yao yatawalaani!
Ndio maana ninamuelewa na kumuunga sana mkono kaka Maxwell Chaila, kupitia programu yake ya Men@Work, inayolenga kumuamsha mwanaume kuyarudia majukumu na nafasi yake halisi. Shida ni kwamba wanaume wengi wanazingatia kile ambacho dunia inasema kuhusu mwanamke badala ya kuishi sawa sawa na NENO (la Mungu) linavyosema kuhusu mwanamke, na hapo ndipo wengi wanapopoteza uanaume wao!
Kama umeupenda ujumbe huu washirikishe na wengine wabarikiwe
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
-
Kuna mafundisho mengi tofauti juu ya Mtu anapokufa, wengine wanasema anaenda kuzimu, wengine jehanamu, wengine peponi, wengine haendi ko...
-
UZINZI UPO HIVI...! 1.Humvunjia heshima mtu na anakuwa na jeraha moyoni. Kwa maana hiyo anakuwa mgonjwa kwa sababu anakuwa kaumia moyo. An...
-
Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wanaume wakisema wanawake wasomi na wenye vyeo ni "wasumbufu". Wengine wamefika mah...

No comments:
Post a Comment