Saturday, 29 April 2017

Mara nyingi hatujali haya mambo ya msingi!

EEH MUNGU NIHURUMIE MIMI MDHAMBI
Nakumbusha! 

Nauliza tu

• Inakugharim kiasi gani kumsalimia mlinzi anaekufungulia geti ukiingia kazini? 

•Inakugharim kiasi gani kumuomba mfanya usafi akuruhusu upite kuliko kukanyaga mahali alipodeki na hapajakauka bado? 

•Inakugharim kiasi gani kumsalimia mtu ambae mmekaa nae seat moja safarini? 

•Inakugharim kiasi gani kusema Asante kama MTU amekutendea vyema?? 

•Wanaume Inakugharim kiasi gani Kusema samahani kwa mke wako unapokosea au unapochelewa kurudi nyumbani? 

•Je Inakugharim kiasi gani kumpakulia mke wako chakula baada ya yeye kupika? 

•Inakugharim kiasi gani kupokea sim na kumwambia mtu Niko ktk mazingira yasiyo rafiki kwa mawasiliano kuliko kuacha sim inaita unaiangalia tu au unakata?

•Inakugharim kiasi gani kumsalimia na kumtendea vyema mtu usiemjua? 

•inakughrim nini kutoa nguo ambazo huzivai na kuwapatia wahitaji, au chakula ambacho kimebaki kuliko kumwaga  kwann usiwape watu wale?

•Inakugharim kiasi gani kupokea sim ya MTU anaekudai na umwambie hujapata pesa yake bado na ukipata utampatia badala yake unazima sim, unabadilisha lain, au unakata sim yake??

•Inakugharim kiasi gani kutenda wema  hata kwa yule anaekuchukia??? 

•kwani inakugharim kiasi gani kumnunulia nguo nzuri house girl/boy wako kukaa pamoja kula pamoja kwann yeye anakula jikoni ninyi mezani? mkitoka outing familia yako na house girl wako, basi mavazi yake na mwonekano wake tu humtambulisha, kwanini?

Ooh Mungu Yehova, wewe uliemwema kwa wingi wa neema yako utufundishe kutenda wema daima! Tuwe kama wewe ulivyo maana wewe ni Baba yetu na sisi ni watoto wako! 

Amen

Bwana akubariki na kukuangazia Nuru ya uso wake, mikononi mwake akutunze daima uwe mwema!

Friday, 21 April 2017

Soma hapa kupata radha ya UZINZI!

UZINZI UPO HIVI...!
1.Humvunjia heshima mtu na anakuwa na jeraha moyoni. Kwa maana hiyo anakuwa mgonjwa kwa sababu anakuwa kaumia moyo. Angalia maneno haya  "Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.Mithali 6:32"

Sasa ukifuatilia hapa utajua kuwa athari za uzinzi ni kuua akili za mtu. Unajua mwanadamu ana akili sana sasa akili zake zikiharibika biblia inasema 

Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, *wayafanye yasiyowapasa*.Warumi 1:28

Sasa kwa maana hiyo Mungu anakuwa hashiriki katika akili zako na kuna mambo yako yote yataanza kufeli.

2. Kupoteza nafasi ya kuoa au kuolewa

 Ikawa baada ya hayo, Absalomu, mwana wa Daudi, alikuwa na umbu mzuri, jina lake akiitwa Tamari, naye Amnoni, mwana wa Daudi, akampenda. Akasononeka Amnoni, hata akaugua, kwa ajili ya umbu lake Tamari, maana huyu msichana alikuwa mwanamwali, Amnoni akaona ni vigumu kumtendea neno lo lote. Lakini Amnoni alikuwa na rafiki, jina lake Yonadabu, mwana wa Shama, nduguye Daudi; naye Yonadabu alikuwa mtu mwerevu sana. Basi Amnoni akalala, akajifanya mgonjwa; na mfalme alipokuja kumtazama, Amnoni akamwambia mfalme Mwache ndugu yangu, Tamari, aje, nakusihi, aniandalie mikate miwili machoni pangu, nipate kula mkononi mwake. Basi Daudi akatuma mjumbe aende nyumbani kwa Tamari, akasema, Nenda sasa nyumbani kwa Amnoni, ndugu yako, ukamwandalie chakula. Amnoni akamwambia Tamari, Kilete chakula chumbani, nipate kula mkononi mwako. Basi Tamari akaitwaa mikate aliyoifanyiza, akamletea Amnoni nduguye mle chumbani. Naye akamjibu, La, sivyo, ndugu yangu, usinitenze nguvu; kwani haifai kutendeka hivi katika Israeli; usitende upumbavu huu. Nami nichukue wapi aibu yangu? Wewe nawe utakuwa kama mmoja wa wapumbavu wa Israeli. *Basi, sasa, nakusihi, useme na mfalme; kwa maana hatakukataza kunioa*. Walakini yeye hakukubali kusikiliza sauti yake; naye akiwa na nguvu kuliko yeye, akamtenza nguvu, akalala naye. Kisha Amnoni akamchukia machukio makuu sana; kwa kuwa machukio aliyomchukia yakawa makuu kuliko yale mapenzi aliyokuwa amempenda kwanza. Amnoni akamwambia, Ondoka, nenda zako. Ndipo akamwita mtumishi wake aliyemtumikia, akasema, Mtoe sasa mwanamke huyu kwangu, ukafunge mlango nyuma yake. Naye alikuwa amevaa kanzu ndefu; kwa kuwa kwa nguo hizo huvikwa binti za mfalme waliokuwa wanawali. Ndipo mtumishi wake akamleta nje, akafunga mlango nyuma yake.
2 SAM. 13:1‭-‬3‭, ‬6‭-‬7‭, ‬10‭, ‬12‭-‬15‭, ‬17‭-‬18 SUV

☝☝Hapo juu unaona kuwa Amnoni alipoteza fursa ya kumuoa binti mzuri Tamari. Na kwa kutokusiliza mazuri. Leo cheki mabinti wengi na vijana wengi wamepoteza nafasi ya kuoa.

3. Kupote

Hapa tunaona Huyu mtu Amnoni alipoteza upendo wake kwa Tamari. Na badala yake chuki iliingia. Maisha tunaishi kwa upendo kwa hiyo chuki kuingia ndio chanzo cha ndoa nyingi kufa.

4.uzinzi unamfukuza Mungu maishani mwako na kwenye ardhi yako. Kwa hiyo unakuwa unaishi bila uwepo wa Mungu kitu ambacho ni hatari sana kwa mwanadamu kuishi bila Mungu.

5.Kuishi kwenye adhabu. Ukisoma hiyo mithali inasema atavunjiwa heshima na mojawapo tunaona kwa Daudi kuwa alipozini na mke wa Uria hakika heshima yake ilivunjwa hadi alitolewa kwenye ufalme. Na kaangalie 2 Samwel 11-12 hapo utaona.kilichompata Daudi. 

6. Maisha ya visasi yaaanza kukuingia. Ndio maana Amnoni alikuwa kuawa na Absolom kaka yale Tamari.

7.Uaminifu unakufa..

8.Ndoto nzuri zinakufa kabisa maishani mwako. Yusufu alipokwepa uzinzi alipewa heshima. Hapa Yusufu wote wawili yule wa Mwanzo kwa Farao na Yusufu aliyemlea Yesu hadi leo anaitwa mtu wa haki.

Mambo ya kufanya sasa.

1.Lazima ujue kuwa nguvu ya upendo ni kubwa sana kwa hiyo lazima ujiepusha kukaa mazingira hatari. Nasema hivi huwezi shindana na nguvu ya upendo kama upendo tu ulimsukuma Mungu kumtoa mwanae mpenzi Yesu. Sasaa je utashindaje wewe? Ndio maana biblia inasema kimbia maana yake ni hatari. 

2.Fanya toba ya dhati kwa Mungu.. na akisaidie ujenge upya..

3.Tumia damu ya Yesu ujisafishe tena na uanze maisha mazuri ndani ya Yesu.

Nakupa home work.

Fanya utafiti kwa watu walioanza zinaa kabla ya ndoa angalia walipo sasa. Wote wameumia na kuumizwa. Na biblia inasema kweli ukiwa mzinzi heshima kwako inaondoka. Na ndio maana utaona wanaume wanapoteza nafasi ya kuwa kichwa ndani ya familia. Wewe fuatailia utaona hiki nonachokuambia.



Sunday, 9 April 2017

NAMNA YA KUPUNGUZA UZITO KWA NJIA SALAMA

NAMNA YA KUPUNGUZA UZITO KWA NJIA SALAMA
Kuna njia nyingi ambazo wengi hutumia ili kupunguza uzito. Kufanya mazoezi ni njia maarufu.

Njia hii inakabiliwa na changamoto zifuatazo:
1. Kukosa muda wa kutosha kufanya mazoezi endelevu

2. Kushindwa kujitawala katika suala la kula na hivyo kuongeza sukari mwilini ambayo kwa kuwa haina matumizi kwa wakati huo mwili huibadilisha na kuwa na fati/mafuta na hivyo kuongeza uzito.

3. Mlundikano wa sumu mwilini. Hii hufanya mwili kushindwa kuendesha shughuli zake ipasavyo.

Japo ni rahisi kupambanana na hali hii kwa kutumia njia zinazokubalika. Njia ambayo itasadia kupambana na changamoto hizo hapo juu ili kuleta mafanikio.

Kupata ushauri na msaada kwa njia ya haraka na salama kiafya, wasiliana na Dr Nature.

Email: real.dr.nature@gmail.com
Phone: +255 767 759 137