Saturday, 27 May 2017
Sababu 5 kwanini wanaume wengi wanachelewa kuoa
1Wakorintho 7:8-9 "Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane, Ni heri wakae kama mimi nilivyo. Lakini ikiwa hawawezi kujizuia, na waoe; maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa".
Ni jambo la kawaida siku hizi kuona Kijana wa kiume anakomaa hadi kidevu bila kuoa, ukiwauliza wanatoa sababu ambazo kwa kweli sio za Msingi, na bahati mbaya sana wanaishia kuwa na ndoa za masaa kwa ajili ya kukidhi TAMAA zao za mwili. Utasikia wakisema "Jamaa kachukua bonge la Mzigo! ", huku binti akifikiri amepata mume kumbe yupo kukidhi TAMAA.
Kuna sababu nyingi zinazowafanya wachelewe kuoa, baadhi ni hizi:
π KUTOJIAMINI AU UOGA WA MAISHA - Vijana mjiamini, ukiwa na uwezo wa kupanga chumba, kupata chakula, kuvaa na mahitaji mengine madogo yanatosha KUOA. Nyumba, Magari, Mashamba, flat screen, Masofa ya kifahari n.k, havina mchango katika kuanzisha ndoa yenye furaha. Mkipata mali pamoja ni vizuri zaidi kuliko mmoja akute kila kitu kipo, zitaishia kuwa ni mali za mtu mmoja.
π SEMENI UKWELI - Wengi wanajifanya kuwa wana uwezo kifedha kumbe hamna kitu, Binti akifuatilia anagundua wewe sio mkweli, anakudharau, uwe kweli, weka mambo yako wazi, itakujengea kujiamini na kuaminika na mwenzio. Wengine ni waoga kutangaza nia, wanaishia kusema "Nampenda sana yule Binti" wenzao wakitangaza nia, wanaanza kuzusha "Yule tayari nilisha onja kumbe muongo", kazi yao ni kuwaharibia sifa mabinti. Wengine, kamwambia tu Binti nakupenda, hata hajapewa jibu, tayari mji mzima wanajua, akija kukataliwa inakuwa aibu.
π KUTOWAAMINI MABINTI - Muda wote wana mtazamo HASI "Negative thinking" juu ya mabinti, kwa sababu alimharibu mmoja, basi kila Binti anayemuona anamdhania sio mwaminifu, anaishia kusema HAPA SIONI wa kuoa. Utakuta mabinti waaminifu wapo ambao hata mende hawajawapitia, lakini vijana wanaishia kusema hawaoni. Kitu cha ajabu unashangaa kaenda KUZOA yeyote, mbali ambako hawajui, na wengine wanajichnganya hadi wa Imani tofauti. Vijana! Tulieni, Oa huyo unayemjua vizuri, utaishia kuoa hadi mshirikina.
π KUTAFUTA BINTI MZURI WA VIWANGO - Kuna Vijana wengi wanajidanganya wakidhani wasichana wazuri kuliko wote ndio wanafaa kuoa, kuna wengi walitumia kigezo hicho walijuta kama sio ndoa kuvunjika. Utasikia vijana wakisema "Reception yake imetulia" huyu ndiye wa kuoa. Wanaanza kugombania na mwishowe wote wanakosa, baada kugundua ni kidumu cha Wenye nazo. Sikiliza; Mungu ameumba kwa namna ya ajabu sana, kila mtu amempatia kitu ambacho mwingine hana, hivyo anayekufaa na kukidhi hitaji lako la Ndoa ni Mungu peke yake anayejua.
Ndio mana kuna usemi usemao "Uzuri wa Mtu uko machoni pa Mtu anayemuona Mzuri", vijana wanatafuta, figure eight, miguu chupa ya bia, macho ya panzi, rangi ya chungwa, maziwa embe dodo nk, hayo yote yanawafanya vijana wengi kuchanganyikiwa na kubaki wanahaha bila mafanikio. Rafiki kuna watu hawana sura wala rangi au umbile zuri, lakini Mungu amewapa ziada vingine ambavyo ukioa hutasikia la Mtu. Ndio utasikia watu wanasema "Hivi huyu kampendea Nini? " siri anaijua yeye. Wengine wanasaka mabinti wasioguswa na mwanaume, bila kujali kuwa wao wameshaguswa, na huku wanamuomba Mungu - kijana mhuni anataka asiyemhuni - huo ni Utapeli.
π UHUNI, vijana wasio waaminifu kwa Mungu wanasukumwa na tamaa za mwili, na kwa sababu wanategemea akili zao, hawawezi kustahimili msukumo wa mwili, wanaishia kuoa kimtindo, anaoa usiku na asubuhi talaka. Hao ndio wanaishia kutangaza Uchumba kwa kila Binti anayemuona, na mabinti wanaishia kubwagwa mara baada kutoa TUNDA, kwa sababu ya kutojua tofauti kati ya TAMAA na UPENDO wa dhati wenye lengo la Ndoa.
Ukiwa mwaminifu Mungu atakupatia bikira safi, mwaminifu utakaye dumu naye milele.
VIJANA WA KIUME MTEGEMEENI MUNGU NAYE NI MWAMINIFU ATAWAPATIA WAKE MTAKAOFANANA NAO.
Ubarikiwe unapochukua hatua.
Kwa masomo zaidi juu ya afya na maisha bora wasiliana +255 767 759 137
Wednesday, 24 May 2017
Tuesday, 23 May 2017
Ujumbe wa tahadhari, mwisho wa dunia
Video hii ni maalumu kwa ajili yako rafiki.
Bofya kuangalia sasa hivi!
Tumefikia mwisho wa wakati. Dunia inakwisha Yesu yauja tena. Jitoe kwake ndugu Yesu anakuita Leo.
Dr Nature 2017
Saturday, 13 May 2017
Kinachotokea baada ya kifo
Kuna mafundisho mengi tofauti juu ya Mtu anapokufa, wengine wanasema anaenda kuzimu, wengine jehanamu, wengine peponi, wengine haendi kokote. Je Mungu anasemaje ?, jibu la kweli tunalipata kutoka katika Neno la Mungu kama lilivyochambuliwa kwenye vipengele vifuatavyo.
(1) MTU AU NAFSI HAI
Mtu au Nafsi HAI ni muungano wa vitu viwili MAVUMBI na PUMZI YA MUNGU, ( Mwanzo 2:7, Ezekiel 18:4 Isaya 53:12 ), Au NAFSI HAI = MAVUMBI + PUMZI YA MUNGU. Hivyo, vitu hivi viwili vikitengana hamna nafsi HAI na ndicho huitwa kifo, mtu anakuwa kuzimu.
(2) KUZIMU KUNA NINI ?
Maandiko yanasema KUZIMU ni sehemu penye ukimya, Mtu aliyekufa au aliyekuzimu hawi na Ufahamu, hivyo hajui lolote juu Mbinguni na Duniani. ( Mwanzo 3:19, Mhubiri 3:18-20, Mhubiri 9:5-6, Zaburi 104:29 ). Pumzi inayomrudia Mungu sio nafsi hai, hivyo inakuwa sawasawa tu na kabla ya mtu hajazaliwa au kuumbwa.
(3) WAKRISTO HALISI HUKIITA KIFO KUWA NI NINI ?
Neno la Mungu linasema kifo ni sawa na USINGIZI, Daudi alikiita kifo kuwa ni USINGIZI WA MAUTI. Kama mtu asivyojua lolote akiwa usingizini ndivyo Marehemu anavyokuwa kabulini hadi kristo atakapokuja. ( Daniel 12:2, Yohana 11:11, Mathayo 27:52, 1Thesalonike4:13, Ayubu 17:13, Luka 8:52-53, Zaburi 13:3, 1Korintho 15:20-23 ).
(4) KUNA UHUSIANO WOWOTE KATI YA WALIOKUFA NA MUNGU ?
Mungu hana uhusiano wowote na waliokufa, kwa sababu hawana kumbukumbu lolote, Pia Kristo alisema Mungu sio wa waliokufa. ( Mathayo22:32, Zaburi 146:1-4 ). Hivyo watakatifu wote waliokufa hawako Mbinguni wamelala kabulini.
(4) NI LINI WATAKATIFU WALIOKUFA WATAONANA NA MUNGU ?
Mbinguni au Peponi wanaenda watu hai au ( NAFSI HAI) wakivishwa miili ya Mbinguni ( Mfano: Eliya, Henoko, Kristo nk. ), Kristo kama alivyotuahidi atakuja kutuchukua pamoja na waliokufa atakapokuja mara ya pili. Tutarudishiwa Pumzi na kuwa hai tena, ndipo tutavishwa miili ya mbiguni na kuanza safari ya kwenda kwa Baba yetu Mbinguni. ( Yohana 5:28-29, 1Thesalonike 4:15-17, Yohana 14:1-3, 1Korintho 15:51-52, Ayubu 14:12, Matendo 24:15, Matendo 2:34 ). Yesu mwenyewe alipokufa msalabani na kuzikwa hakuenda mbinguni hadi alipofufuka ( Yohana 20:17 )
(5) LINI WAOVU WATAINGIA JEHANAMU ?
Waovu wataingia Jehanamu baada ya Kristo kupitisha hukumu, Ni ahadi ya kristo pia kuja siku ya mwisho kuuhukumu ulimwengu na kutoa adhabu ya Moto. Waovu watafufuliwa katika ufufuo wa pili, wote watakuwa hai na kudhihirishiwa matendo yao yote, ndipo MOTO utawashwa kwa ajili yao. ( Ufunuo 6:14-17, 20:13-15, 22:12, Mathayo 16:27, 2Petro3:7-10, Isaya 25:9, Yohana 5:28-29, Mathayo 25:31-41, Malaki 4:1, Rumi 2:5-6 ).
Viongozi wa dini wanaofundisha kuwa Mtu akifa hapohapo anaenda Jehanammu (Motoni) au Peponi (Mbinguni) ni lazima tuwaangalie sana huenda kwa kujua au kutokujua wanatumiwa na yule adui kwa hila kuvuruga ukweli halisi juu ya mpango wa Mungu Kuuhukumu ulimwengu kwa haki kama Injili inavyosema.
MAFUNGU YA BIBLIA YANAYOTUMIWA KUPOTOSHA UKWELI
WAEBRANIA 9:27.
Kama tulivyosoma hapo juu baada ya Kifo hakuna kinachoendelea, yaani mtu hana nafasi tena ya kuamua kufanya mema au mabaya. Kilichoandikwa kitabuni mbinguni dakika ya mwisho ya kukata Roho, ndicho kinapelekwa hukumuni siku ya mwisho Kristo atakapokuja. Mtu akifa rekodi za matendo yake zinafungwa tayari kwa hukumu. Pia neno la Mungu linasema hukumu kwa waliokufa imeshaanza, hii inaitwa hukumu ya upelelezi ambapo vitabu vya kumbukumbu kwa waliokufa vinapitiwa mmoja baada mwingine hadi siku ya Mwisho.
LUKA 23:39-43.
Hapa Kristo alikuwa anamhakikishia mhalifu kuwa watakuwa wote peponi, Neno halijasema "LEO HII" Kristo amesema "LEO HIVI". Hapo kuna makosa ya uchapaji na tafsiri kutoka lugha ya awali ya kigiriki, alama ya koma (,) kwa kiswahili sahihi haijawa mahali pake. Hata hivyo kama tulivyosoma Kristo alithibitisha kuwa hakuenda Mbinguni (Peponi) alipokufa ( Yohana 20:17, Yohana 14:1-3 ). Pia ukumbuke kuwa Mungu sio kigeugeu na neno lake halipingani.
LUKA 16:19-28.
Mfano huu wa Tajiri na Maskini Lazaro, umekuwa ni kigezo kikubwa cha Shetani kutumia kuwavuruga watu washindwe kuielewa Injili na ahadi za Kristo. Kabla ya kutoa maelezo juu ya mfano huo soma na kutafakari mifano mingine iliyotolewa na Kristo ( mfano: Luka 16:1-15 ) Je unaweza kusema "Kristo alihalalisha mali ya Udhalimu ? ", Mifano iliyotolewa kwenye Biblia, kabla hatujaichukuwa kama mafundisho, ni lazima tuangalie vitu vufuatavyo : Mfano ulitolewa na nani, Kwa watu wa aina au hali au Tabia gani, Dhumuni au Fundisho maalumu la mfano, na Je biblia nzima inasemaje juu ya Fundisho hilo.
Katika mfano huo Fundisho au Dhumuni lilikuwa juu ya hali halisi ya Matajiri wenye Ubinafsi na Maskini, itakavyokuwa wakati Kristo atakapokuwa akimlipa kila mtu mshahara wake. Kristo hakuwa na maana kuwa mtu akifa anakwenda Peponi au Jehanamu halafu wanakuwa wanawasiliana. Shetani anajua kuchanganya ukweli na uongo lakini kwa kuichambua biblia nzima kwa msaada wa Roho mtakatifu, siri zote za muovu zinafichuliwa. Watu wengi leo wamechanganyikiwa hadi wanasema biblia inajipinga.
MAFANIKIO YA SHETANI KUPITIA SOMO ZIMA LA WAFU
[A]
Shetani amefanikiwa kueneza uongo wake aliousema kwa mama yetu EVA katika Bustani ya Edeni. Mungu alisema "hakika mtakufa", Shetani alisema "hakika hamtakufa". Hata hivyo Mungu kwa njia ya manabii, Kristo na Mitume amezidi kuthibitisha kuwa Binadamu sharti afe, Kufa ni Amri tangia Edeni. Na shetani anaendeleze uongo kuwa Mtu hafi ila anabadilishwa mwili na kuwa na nafsi hai.
[B]
Amewaingiza wengi kwenye Ibada za Umizimu bila kujua. Kuomba, Kuongea na Wafu na kuwaombea wafu ni Ibada za Umizimu, Kwa kuamini kuwa Wafu wako mbinguni, Shetani anajigeuza na kuja kwa sura za watakatifu waliokufa na kuwaagiza watu wamwabudu Mungu kwa njia ambazo zingine ni kinyume na Maandiko. Ibada ya Sanamu, Lozari na sadaka ya wafu walioko pagatori ni baadhi ya mafundisho yaliyoingizwa kanisani kwa hila ya mwovu na wengi hawajui. Kuomba au kuwaombea Wafu Ni machukizo kwa Bwana ( Kumbukumbu la torati 18:9-12 ).
[C]
Amefanikiwa kueneza Imani ya Pagatori, ambayo amewafanya mamilioni ya watu wapotee, kwa kutojiandaa wakiwa Hai, wakitegemea kuja Kuombewa na kutolewa sadaka ya msamaha na ndugu zao walio hai ili watoke Pagatori na kwenda peponi.
[D]
Amewafanya wengi wachanganyikiwe wasielewe sawasawa Ahadi za Kristo juu ya Kurudi mara ya pili kuja kuuhukumu ulimwengu, na Injili kuhusu Kiama imevurugwa. Pia amewaminisha wengi kuwa Mungu si wa HAKI kwani anawapeleka Jehanamu kabla ya, Hukumu na wenye Mapesa wanaweza kumlipa wakasamehewa wakiwa pagatori, hivyo kumfanya Mungu kuwa anaupendeleo.
Ndugu yangu inakupasa uchague leo kuwa katika wokovu wa kweli au wokovu ambao Kristo aliuita wa watu
wapumbavu, yaani wale wanaomkiri Kristo kuwa mwokozi wao kwa midomo tu ila wanakataa kutii Neno lake.
Yesu anakuita kwa Upole na kukutahadharisha, Fanya uamuzi sasa.
[ Mathayo 7:24-27 , Ufunuo 18:4-5 ]
Ubarikiwe sana.
Wednesday, 10 May 2017
Tahadhari video na picha za ngono
Elewa kwamba XVIDEOS ni video za ngono ambazo pia hujulikana kama Mikanda ya X, na XPICTURES ni picha za uchi zilizopigwa na watu mbalimbali kote ulimwenguni ambapo nyingi kat yazo hupigwa na wanawake.
Sasa leo nataka kukujuza jambo hili, ya kuwa Amin usiamin ndugu yangu ukwel ni kwamba si video zote za ngono huchezwa na watu wa kawaida, zipo ambazo huchezwa na evil spirits kama vile ‘majini’ ambayo huchukua umbo la mtu na kuonekana kama mtu wa kawaida. Nadhan wote tunajua ‘majini’ ni roho na roho hizo zinauwezo wa kujivika maumbo ama miili ya vitu mbalimbali ikiwemo miili ya wanyama au hata miili ya wanadamu, jambo ambalo huweza kufanywa pia na wachawi wa viwango vya juu.
Kumbe bas unaweza kutazama video hizo au picha hizo za uchi ukizan unawatazama wanadamu wa kawaida kumbe ukawa unatazamana live na majini yaliyochukua shape za watu. Na kwa kutazama huko ndipo unakuwa umefungua mlango kwa roho hizo kukuingia wewe na kukutumikisha kadri zipendavyo. Na roho hizo za kishetani zinapomwingia mtu humfanya kuwa mtumwa wa video hizo.
Watu wengi wamekuwa wakitazama video hizo kwa kisingizio cha kujifunza style mbalimbali za ufanywaji wa tendo hilo! Je ni kweli nuru yaweza kujifunza kitu chema katikati ya giza? Au ni mkristo yupi kati yetu anayeweza kutuambia ni wapi Adamu na Eva walipojifunza ama kutazama ufanywaji wa tendo hilo hata wakawazaa Kain na Abeli?
Ndio maana leo hii wapo wengine wenye ndoa zao lkn hawapati tena msisimko wa mwili kwa kuwatazama wake zao hadi pale watakapotizama video hizo au picha hizo, je huu sio utumwa? Lakini pia sote tunajua ya kuwa ukimtizama tu mwanamke kwa kumtaman tayari unakuwa umezini nae rohoni mwako, je waweza kwel kuikwepa dhambi hii pale unapotazama picha na video hizo chafu?
Wengine wameishia kujifunza ufanywaji wa tendo hilo kinyume cha maumbile yaani anal sex kisha kuwalazimisha wenzi wao kufanya kwa kupitia njia hiyo, je Mungu hakukataza mambo hayo?
Wapo pia wafanyao homosexual (yaani watu wa jinsia moja) au group sex ( mwanaume mmoja akiwa na wanawake zaid ya 1 au mwanamke m1 akiwa na wanaume zaid ya m1) nk. Je twaweza kujifunza kitu gani chema toka kwa watu hao wafanyao mambo hayo ya sodoma na gomora?
Au uliwahi kuona video hata 1 kat ya hizo wachezaji wake wanaanza kwa sala ya kumwomba Mungu na kisha wakahitimisha japo hata kwa maombi mafupi?
Ajabu utumwa huo leo umewafanya watu wengine kuficha video hizo na picha hizo kwenye laptop zao, desktop, ipad au hata kwenye simu zao na kulock mafile hayo kwa kuyawekea password au majina ya kujua wao , lakni je unapofanya hivyo unakuwa unamficha nani hasa? Je unazan wakat unahide mafolder hayo Mungu huwa hakuoni? Ni kweli unaweza kuwaficha wanadamu lakini je waweza pia kumficha hata Mungu wako?
Neno la Mungu katka Warumi 1:28-32 linasema watu wanayajua mambo yote maovu yawapasayo hukumu lakini pamoja na kuyajua kwao bado wanayafanya mambo hayo na wale wasiyoyafanya wanakubaliana na wale wayafanyayo.
Mf pengine kweli wewe hufanyi anal sex,group sex au hufanyi kabisa zinaa lakini unakubaliana na wafanyao zinaa kwa kuwatazama au hata kwa kuwahifadhi kwenye PC au simu yako, je hujui kwa kufanya hivyo unakuwa huna tofauti yeyote na wao?
Pole sana ndugu yangu kama na wewe u miongon mwa watu wengi wanaotumikishwa na roho hizo chafu.
Chakufanya: We fanya toba ya kwel na umwombe Mungu msamaha huku ukikusudia kuacha, kisha futa na udelete kabisa video ama picha hizo mahali popote ulipozihifadhi kisha mwombe Mungu akusaidie kuikimbia zinaa na pia epuka mazingira ya ukiwa au namna yoyote yanayoweza kukusabisha kutumbukia humor
. Kumbuka “Aonywae mara nyingi akishupaza shingo, atavunjika ghafla wala hatapona tena (Mithali 29:1)
Wako akupendaye,
Yusufu Mohamed Filemon
Dr Nature
Tuesday, 9 May 2017
Ulifahamu hili kuhusu Easter?
SIKUKUU YA EASTER
____________________________________
π΄Hebu tuone CHIMBUKO LAKE.
*Pasaka kwa kigiriki ni* "Pasach" sawa na
*>>kiebrania* "Pasach". *>>Kwa kiingereza* ni
Passover.Hivyo kwa tafsiri ya Biblia pasaka sio
"Easter".
π΄ Pasaka ni sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu
Matendo 12:1-5.
Neno " Pasaka " kwa kiingereza ni "
Passover "
maana yake "kupita juu ya... "
*π΄ Katika Agano la kale pasaka inazungumzwa kuwa* :.M
ungu alimuagiza Musa kupaka damu katika miimo
ya milango ya Waisraeli wakati malaika AKIPITA kuangamiza wazaliwa wa. Kwanza wa wote wasio kuwa na hiyo alama ktk milango yao.
.....Kwa Waliopaka malaika alipita juu ya nyumba zao bila kuangamiza, waliokiuka alipita ndani na kuangamiza.
π΄ Kutoka 12:12-14; KJV.inasema "...i will
pass over you and the plague shall not be upon
you to destroy you.....And this day shall be unto
you for a memirial.
Hivyo pasaka ni kumbukumbu ya wana wa Israel toka
utumwani misri.
na Mungu akaagiza iendelezwe
hata nchi ya ahadi kanani.
π΄ Leo sisi ni Israeli ya kiroho tunaadhimisha kutoka
*Misri ya utumwa wa dhambi kwenda kanani ya mbinguni.*
......Katika Agano jipya 1Wakorintho 5:7-8. Basi
jisafisheni mkatoe ile chafu ya kale ...
....kwa
maana PASAKA wetu amekwisha kutolewa kuwa
sadaka yaani kristo......
Hakuna andiko linaloagiza utunzaji wa,"Easter"
kama pasaka.
hili la EASTER limetoka wapi?.
*_πΊUKWELI JUU YA EASTERπͺ_*
___________________________
π΄ Jina EASTER linatokana na "Ostera"
au"Eostre" ambaye ni. goddness of sprin
(mungu wa mavuno)
katika nchi za Anglo-
Saxon,
... Babeli anaitwa "Ishtar",
Syria anaitwa
"Ashtaroth",
Kiebrania anaitwa "Ashtoreth",
Kigiriki anaitwa "Eostre"
Germany anaitwa "Ostera"
"Ishter" hutamukwa. "Easter"
π΄ Hii ni siku ya mungu
*"Tamuz"* ambaye ni mtoto wa pekee wa mungu
jua na mungu mwezi
Nimrod ni mjukuu wa Nuhu kwa kijana wake
Ham.
Ham alikuwa na kijana aitwae Kushi.
Kushi
alioana na Semiramis wakapata mtoto anaitwa
*>Nimrod<*
Baada ya kifo cha baba yake Nimrod akamuoa mamayake mzazi Semiramis akawa mtawala
mwenye nguvu sana.
Soma> Mwanzo 10:8-10)
π΄ Siku moja Nimrod alienda vitani na akauawa na
adui zake
...Semiramis akasema Nimrod ameenda juu
kwenye jua hivyo akaitwa Baal yaan mungu jua
(the goddnes of sun).Semiramis akaagiza
*akumbukwe kwa kuwasha mishumaa wakati wa ibada* (ndivyo wanavyofanya madhehebu mengi mpaka leo)
π΄ Semiramis akajiita "Ishtar"(easter)
*mungu mke*
"moon goddnes".
Huyu "Ishtar " akatembea na
kijakazi wake akapata mimba akasema kapata
mimba ,kupitia " Sun rays(miali ya jua)" kutoka kwa
"BAALI (Nimrod) ambaye alikuwa
*mungu JUA au mungu mume.*
Akazaa mtoto akamwita " Tamuz ".
π΄ Kijana huyo l (Tamuz) baadaye aliuawa na Nguruwe pori
alipokuwa akiwinda.
"Ishtar" *ANAABUDIWA kama "mother of god and queen of heaven".*
Ndivyo walivyofanya wengi hadi leo."Ishtar" wanamwita Bikira Maria.
π΄ Baada ya kifo cha
Tamuz, mama yake
akatangaza siku 14 za maombolezo akap
iga *MARUFUKU ULAJI wa NYAMA* ktk Maombolezo hayo
......ndivyo wanavyofanya wengi ktk
Siku ya IJUMAA *(ijumaa kuu)* kabla ya Jumapili ya Easter" hawali nyama.
*...Tukio Hilo limevikwa hadhi ya KUMBUKUMBU YA MATESO YA YESU.*
Tazama hii:
Every year on the first
Sunday after the first full moon after the spring
equinox a celebration was made until today).
"Ishtar/Ashtoreth" is queen of Heaven,
*π΄ EASTER ni kumbukumbu ya TAMUZ "*
Tuwe makini na mafundisho yasiyo ya KWELI.
>>Ktk Waamuzi 2:11-13-inazungumza taifa lilivyo asi
na kumwabudu *"Baal"*
.>>1Samwel 7:3-4-Waisraeli waligeukia Baali na
*Ashtoreth*
>>1Wafalme 11:4-6-Suleimam alivyomuoa
mwanamke wa kimataifa akamgeuza na kuabudu
*"Ashtoreth"*
π Kwa maelezo ya ziada pitia hiki kitabu:
*_>>The Easter Celebration - History of Its Hidden Origins_* (Traditions of North America and the Western World Book 1)
>>Ni vyema kuugeukia ukweli wa BIBLIA<<
π΄ Baada ya kuona ukweli huo, Naomba ambaye hajapata SOMO la *"PASAKA ILIYOFANYWA NA YESU "*
Ubarikiwe unapowashirikisha wengine ujumbe huu.
Sunday, 7 May 2017
How to set sexual boundaries in 21st century
SET SEXUAL BOUNDARIES!
(For all Christians: pastors, deacons, deaconesses, elders, dep'tal leaders, members)
“I made a covenant with my eyes; how then could I entertain thoughts against a virgin? (Job 31:1, NET BIBLE')
Sexual immorality is on the increase all over the world. Adultery is fast becoming the norm and men of God are also joining the club. Married women are not left out, many are having secret lovers and emotional affairs are becoming the order of the day.
The rate at which immorality is increasing is alarming! It is spreading fast into every nook and cranny and children are also being initiated into the club. It's no news that 4, 5 years old kids now have sex with each other. Staying sexually pure these days is becoming a Herculean task.
One of the reasons people fall flat into illicit sex is over confidence. The stupid belief that you can be free around the opposite sex and nothing would happen!
A lot will happen! One of the ways you can stay sexually pure whether married or single these end time is to set strict boundaries. If you are too careless around the opposite sex, you will fall flat on your face! That is the truth. The ealier you believe this and work on it, the better. You can't be careless around the opposite sex and hope to stay sexually pure, set boundaries!
There are some people who can't be your friends, raise the standard. Any body can call you names, that's their headache, you have your destiny to protect. As a rule, I don't make friends with liars, gossips and jealous people. They make life so complicated. If you believe in illicit sex, we can't be friends, period!
Monitor your chats. Don't allow anybody send you flirty messages, no matter how innocent it sounds, warn them and if they refuse to stop, block them!
Limit the hugs and touches. I don't hug women as a rule. If I must hug, my wife must be around and you should hug both of us. If your hugging anointing is only for me, I want none of it.
Don't allow anybody call you pet names (except your close family members and same sex friends), it doesn't make any sense. Pet names turn the opposite on, if you don't know that, know it right now.
Be sensitive to attractions. Don't be naive around the opposte sex, know when a man/ woman is sexually attracted to you and move back from that person. If they focus too much on your physique and body, they are sexually attracted to you, move back.
Know when you are sexually attracted to someone and move back. It's perfectly normal to have chemistry for someone. Marrying the greatest man on earth or the most beautiful, virtous woman in the universe will not automatically stop you from being attracted to someone else. Know when the thought of another man/ woman get you excited and move back.
Don't jump at new relationships. Give it time. Study the person, know what they stand for, see if your core values are compatible, if not, move back!
Leadership attracts all kinds of people. If you are a leader or you are gifted, talented or intelligent, the opposite sex will show more interest in you, be careful whom you allow to get close to you.
Accepts gifts with care. Men don't joke with their time and money. If he spends so much time and money on you especially when you do not ask, he may one day ask for sex. Stop begging men for money. Work with your two hands and raise your standard. Men will respect and honour you for it.
Work on your marriage. Fix the problem as soon as possible or else you get attracted to someone who gives you what you lack in your marriage, adultery is the result.
Be prayerful, be watchful. Jesus says "watch and pray that ye may not fall into temptation..."
Don't stay with the opposite sex in a dark or lonely room.
Don't counsel the opposite sex on a bed in a lonely room.
Avoid provocative dresses and pictures. Let your spouse or parents advise you on what is okay for you.
Mind the pictures you post on the social media, if it is getting unecessary opposite sex attention, delete it.
Don't visit the opposite sex alone, especially at night. It doesn't make sense.
These and more are the things you need to do to stay sexually pure in this 21st century.
People may laugh at you, it doesn't matter. They may call you a neurotic, psychotic, fanatic, over sensitive or paranoid, don't give a damn! Your destiny is too precious to waste on the altar of sin. Avoid friends who make fun of holiness and make friends with people who appreciate purity and holiness.
Finally, avoid the second look, as far possible. I agree perfectly with Job on his resolution never to look lustfully at any lady. Yes, you can avoid the second look.
Your lovely doctor,
Yusuf Mohamed Filemon
[Dr Nature]
0767759137
©2017

Monday, 1 May 2017
Jifunze kukokotoa tarehe za matukio
JIFUNZE KUHESABU TAREHE, JUA HATA PASAKA YA MWAKANI ITAKUWA TAREHE NGAPI?
KALENDA za mwanzo ziliutumia mwezi wa
angani kama kipimo cha muda. Ziliitwa “Lunar
calender” au Kalenda-Mwezi. Tarehe 1 ya
Mwezi ilikuwa ni siku ulipoandama yaani
Mwezi-Mdogo (Crescent Moon).
Mwezi unapofika siku ya 15 unakuwa umefikia
ukubwa wa juu na huitwa Mwezi-Mkubwa (Full
Moon). Hivyo kwa kalenda ile tarehe 15
ilikuwa ni siku ya Mwezi-Mkubwa.
Mwaka 45KK, Julius Caesar alitangaza kalenda
mpya ikaitwa “Julian Calender” iwe na siku
365. Wakati huo ikijulikana kwamba jua
huzunguka kwa siku 365.25. Hivyo pengo la
kalenda na mzunguko likabaki robo siku.
Robo hiyo ifidiwe kila baada ya miaka minne
mwishoni mwa mwezi Februari ambayo sasa
ulifanywa kuwa wa pili baada ya January.
Inapofanyika hivyo, huo ukaitwa mwaka-mrefu
(Leap year).
Mwaka mrefu ukachaguliwa kuwa ni ule tu
unaogawanywa kwa nne mfano miaka ifuatayo
1700, 1800, 1900, 2100, 2200, 2300.
Baadaye iligundulika kuwa dunia huzunguka kwa
siku 365.24218967 ziitwazo “Tropical year”.
Hizi ni chache kuliko siku 365.25
zilizokadiriwa mwanzoni. Uchache huu
husababisha kuwe na pengo la dakika 11 na
sekunde 14.812512 kwa mwaka.
Pengo hili ni dogo, lakini hupanuka hadi kuwa
siku nzima kila baada ya miaka 128.0355.
Mwaka 1545 lilivuka siku 9.25.
Kuondoa tatizo hili, Papa Gregory XIII aliamuru
iundwe kalenda mpya na akachagua Oktoba
04, 1582 iwe siku ya mwisho kutumika “Julian
Calender”. Kesho yake, kalenda mpya ikaanza
kutumika. Ungetegemea hiyo kesho iwe ni
Oktoba 05, 1582. Lakini ili uzibe pengo lile
lililofikia siku kumi, ilibidi kalenda mpya
kuziruka siku hizo siku kumi. Hivyo hii mpya
iliyoitwa “Gregorean Calender” ikaanza kama
Oktoba 15 badala ya Oktoba 05.
Ndiyo sababu katika historia ya nchi nyingi
Ulaya, hakuna tarehe za Oktoba 05, 1582 hadi
Oktoba 14, 1582. Watu walilala Oktoba 04,
1582 kesho yake wakaamka ikiwa ni Oktoba
15, 1582.
Teresa Alonso huandikwa kwamba alifariki
Oktoba 1582, kwenye usiku wa tarehe NNE
kuamkia tarehe KUMI NA TANO! Alipotangazwa
kuwa Mtakatifu, Kanisa Katoliki likaifanya
Oktoba 15 kuwa siku ya kumkumbuka, yaani
siku ya Mtakatifu Teresa wa Avila.
Usipofahamu kwamba Mtakatifu Teresa alifariki
siku kalenda zinabadilishwa, utadhani
aliyeandika vile tarehe za kifo chake
amekosea!
Waandishi, William Shakespeare wa Uingereza
na Miguel de Cervantes wa Spain huandikwa
kwamba wote walifariki Aprili 23, 1616. Lakini
ukweli ni kwamba hawakufa siku moja bali
walipishana siku kumi kwani England
ilichelewa kwa karibu miaka 200 kuikubali
“Gregorean Calender”!
“Gregorean Calender” haikuundwa ili kuishia
kuliziba lile pengo. Bali pia, kuhakikisha
halitokei tena. Tumeshaona kuwa lile pengo ni
dakika 11 na sekunde 14.812512. Hivyo,
linapanuka na kuwa siku tatu ndani ya miaka
400.
Hivyo kuliziba inatakiwa kupunguza siku tatu
kila baada ya miaka 400. Je, zipunguzweje?
Kipande cha miaka 400 kina miaka mitatu ya
karne inayogawanyika kwa 4 lakini
haigawanyiki kwa 400.
Ikakubalika kwamba unaogawanyika kwa 4,
lakini haugawanyaiki kwa 400, usiendelee
kuwa mrefu. Humo siku moja ichomolewe na
uwe mfupi.
Ndipo miaka 1700, 1800, 1900 haikuwa tena
mirefu. Ndivyo pia miaka 2100, 2200, 2300
nayo haitakuwa mirefu. Kwa sababu ni miaka
ambayo “Gregorean Calender” inachomoa siku
moja ili kutosababisha pengo tena.
Kipande hiki cha miaka 400 kikaleta wastani
mpya wa siku 365.2425 kwa mwaka. Sasa lile
pengo lile la siku moja si rahisi kufikiwa.
Kwenye “Julian Calender” tumeona lilikuwa
miaka 128.0355 lakini sasa limekuwa miaka
3,222.
Sasa tuijadili tarehe ya siku ya Pasaka tukiwa
na ufahamu wa kalenda zile. Je, tarehe ya
Pasaka imetajwa ndani ya Biblia? Kuna kifungu
kinasema hivi:
“..Mwezi wa kwanza, siku ya kumi na nne ya
mwezi, wakati wa jioni, ni Pasaka ya BWANA.
Na siku ya kumi na tano ya mwezi huohuo ni
sikukuu ya BWANA, ndiyo siku ya mikate
isiyotiwa chachu. (Walawi 23:5)..”. Hivyo
Pasaka ni tarehe 15 ya mwezi wa Kwanza.
Lakini Biblia pia inautaja mwezi wa kwanza
kwa jina la Nisan (Esta 3:7, Nehemia 2:1).
Yesu alisulubiwa mwaka ambao Ijumaa
iliitangulia sikukuu ya Pasaka kwa siku moja
(Yohana 18: 28, Marko 15:42-43). Hivyo
tarehe ya Yesu kusulubiwa ni Ijumaa, Nisan
14. Siku moja kabla ya Nisan 15. Siku moja
kabla ya Mwezi-Mkubwa.
Baada ya Yesu, Wakristo wengi Pasaka
waliiadhimisha Jumapili, lakini utata ulijitokeza
kuhusu tarehe ya kuiweka hiyo Jumapili ya
Pasaka. Ilifika wakati jimbo moja la Wakristo
linaadhimisha siku tofauti na jingine na kwa
njia wanayoijua wao.
Utata huu uliondolewa kule Nicaea mwaka 325
ambapo Kanisa Katoliki lilipoamua kuwa,
tarehe ya Pasaka iwe moja tu duniani kote,
yaani iwe ni Jumapili inayokuja baada ya
Mwezi-Mkubwa (Full Moon) unaotokea baada
ya siku ya Ikweta, yaani baada ya Machi 21
(Equinox).
Baada ya uamuzi huu, wataalamu walipania
kuunda chati maalum zenye tarehe za Mwezi-
Mkubwa zitazokasaidia kuitambua tarehe ya
Pasaka kwa mwaka wowote.
Mwezi huizunguka dunia kwa siku
29.5305891203704 (Synodic Month), wakati
dunia hulizunguka jua kwa siku 365.24218967
(Tropical year).
Mizunguko hii miwili ikianza safari siku moja,
itapishana kila mwaka, lakini itakutana tena
mwezi unapokamilisha mizunguko 235.
Dunia
nayo inakuwa imekamilisha mizunguko 19,
yaani miaka 19.
Wataalamu wakaitumia hii miaka 19
kutengeneza chati yenye tarehe za Mwezi-
Mkubwa unaotokea March 22 hadi April 18.
Tarehe zile zikaitwa tarehe za Mwezi-Mkubwa
Wa Pasaka au Ecclesiastical Full Moon (EFM).
Ndani ya ile miaka 19, kila mwaka ukapewa
tarakimu iitwayo Golden Number inayosimama
badala ya mwaka ikiwa na tarehe zile
ziliorekodiwa za Mwezi Mkubwa wa Pasaka.
Chati yenyewe ya Golden Number na tarehe
zake (siku/Mwezi) ni hii ifuatayo: {1=5/4,
2=25/3, 3=13/4, 4=2/4, 5=22/3, 6=10/4,
7=30/3, 8=18/4, 9=7/4, 10=27/3, 11=15/4,
12=4/4, 13=24/3, 14=12/4, 15=1/4, 16=21/3,
17=9/4, 18=29/3, 19=17/4}
Golden Number ya mwaka inapatikana kuanza
kuugawa mwaka kwa 19. Tulifundishwa
mashuleni kuwa namba inayosalia baada ya
kugawa huitwa “Baki” . Hii “Baki” ukiijumlisha
na 1 unapata Golden Number (GN).
Mfano unatafuta GN ya 27. Hatua ya kwanza ni
kutafuta “Baki” baada ya kugawa 27 kwa 19.
Hizi ni hesabu za “modulo” , yaani zinahitaji tu
namba inayobaki baada ya kugawa.
Ikiandikwa hivi: (27 mod 19) inatakiwa namba
inayobaki baada ya kuigawa 27 kwa 19. Jibu
ni 8. Hivyo tulipaswa tuandike hivi: (27 mod
19=8). “Baki” 8 tuliyoipata, ndiyo tunaihitaji ili
tuijumlishe na 1 ili tupate GN ambayo hapa ni
9 kwani (8+1=9).
Tungeweza pia kuandika hivi : 27 mod 19 +
1=9. Hivyo kanuni ya kupata GN kwa mwaka
wowote ni hii:
(MWAKA mod 19 + 1). Yaani, ugawe huo
mwaka kwa 19, kisha namba itakayobaki
ijumlishe na moja.
Ukishaipata GN, itafute kwenye ile chati
ambapo utaiona ikiwa na mwezi na tarehe.
Jumapili inayofuata baada ya tarehe hii ndiyo
tarehe ya Pasaka ya mwaka huo.
Tutumie chati ile na kanuni hii kujua tarehe ya
Pasaka ya mwaka 1474. GN ni (1474 mod 19
+ 1=12). Hivyo GN ni 12.
Kwenye chati, 12 inaonyesha ni tarehe 4/4.
Hivyo, mwaka 1474 Mwezi-Mkubwa wa
Pasaka ulikuwa tarehe 4/4/1474. Hiyo ilikuwa
ni Jumatatu. Hivyo Pasaka ilikuwa ni Jumapili
iliyofuata yaani tarehe 10/4/1474.
Lakini, Kanisa Katoliki liliikubali kanuni hii
karne ya sita. Hii ndiyo sababu, tarehe za
Pasaka zinazojulikana ni zile tu zinazoanza
mwaka 533.
Ndivyo Pasaka ilivyotafutwa miaka ile. Sasa
tuone Pasaka ya kizazi chetu. Kizazi cha
“Gregorean Calender” iliyoanza mwaka 1582.
Tumelijadili lile pengo la siku lililofikia ambalo
mwaka 1582 lilishafika siku 10. Ukweli ni
kwamba kabla halijazibwa, Pasaka ilikuwa
inawadia lakini uhalisi ni kwamba inakuwa
tayari imepitwa siku 10. Kinyume kabisa na
maamuzi ya Kanisa kule Nicaea!
Ili kulizuia lisitokee tena, tumeona uchomoaji
wa siku moja toka kwenye miaka inayofunga
karne, isiyogawanyika kwa 400. Uchomoaji
huu umewekwa kwenye kanuni (formula)
iitwayo “Solar Equation”.
Kama mwendo wa kuzunguka jua
umezingatiwa na “Gregorean Calender”, vipi
kuhusu mwendo wa mwezi?
Tumeuona kwamba mizunguko ya mwezi na
dunia hukutana kila baada ya miaka 19.
Kadirio la dunia kuzunguka kwa siku 365.25
linafanya ikizunguka kwa miaka 19 zinakuwa
siku 6,939.75. Mwezi utakuwa nao
umezunguka mara 235, huku kila mzunguko
ukitumia siku 29.5305891203704.
Hivyo, kukutana kule ndani ya kila miaka 19,
huleta pengo dogo la saa 1, dakika 28,
sekunde 38.5.
Mapengo madogo haya tunayoyapuuza
mwanzoni, yameshatugharimu vya kutosha.
Pengo hili kwa mwaka ni dogo lakini kwa
miaka 2500 linakuwa hadi kufika siku nane.
Kwenye hesabu za kutafuta Pasaka
urekebishaji wa hili pengo hutokea kwenye
kanuni iitwayo “Lunar Equation”. Lakini kwa
sababu ya tofauti ya uelekeo wa mzunguko wa
mwezi na dunia, “Lunar Equation” hujumlisha
mara nane kila baada ya miaka 2500.
Hivyo, mahesabu yoyote ya kuitafuta tarehe ya
Pasaka hayakosi kanuni hizi mbili “Solar
Equation” na “Lunar Equation” .
Tumeona kwamba kalenda ilianza mwaka
1582. “Solar Equation” inaondoa siku moja
toka kwenye miaka 1700, 1800, 1900. Hivyo,
ni kujidanganya kusema kwamba miaka yote
inayogawanyika kwa nne ni mirefu, jambo
ambalo hata mimi nilifundishwa shuleni. Hapa
tumeona kwamba “Solar Equation” imeondoa
siku moja kwenye mwaka 1900 na hivyo
haukuwa mwaka mrefu ingawa unagawanyika
kwa nne.
“Lunar Equation” huongeza siku moja kwenye
miaka 1800, 2100, 2400. Mwaka 1800
unaguswa na vyote “Solar Equation” na “Lunar
Equation”. Hivyo hauathiriki.
Kanuni zote za kuitafuta Pasaka huzingatia
zaidi ya niliyoyaeleza, lakini cha muhimu zaidi
ni hizi mbili yaani “Solar Equation” na “Lunar
Equation” ambazo sijawahi kuzisikia kwa
kiswahili.
Ni vigumu kuepuka hesabu za “modulo” au
“mod” unapotafuta tarehe ya Pasaka. Lakini
ukiwauliza wanafunzi wa darasa la nne
kwamba machungwa 2011 yakipangwa kwenye
mafungu 19, ni mangapi yatakosa fungu?
Wapo watakaopata jibu sahihi kwamba ni
machungwa 16. Kimahesabu swali hilo
linaandikwa hivi: (2011 mod 19) na jibu lake
ni 16, yaani (2011 mod 19=16).
Ifuatayo ni moja ya kanuni zinazotumika
kuipata tarehe za Pasaka ya mwaka wowote
kuanzia 1700 hadi 2099:
(1) : a=MWAKA mod 19;
(2) : b=MWAKA \ 100;
(3) : c=MWAKA mod 100;
(4) : d=b \ 4;
(5) : e=b mod 4;
(6) : f=c \ 4;
(7) : g=c mod 4;
(8) : h=(b + 8)\25;
(9) : i=(b – h + 1)\3;
(10) : j=(19xa + b – d – i + 15) mod 30;
(11) : k=(32 + 2xe + 2xf – j – g) mod 7;
(12) : m=(a + 11xj + 22xk) \ 451;
(13) : n=j + k – 7xm + 114;
(14) : Tarehe=(n mod 31) + 1
(15) : Mwezi =n\31;
Penye neno MWAKA, andika mwaka unaotafuta
kujua tarehe yake ya Pasaka. Panapotokea
alama (\) ni kugawanya ambako hata kama
jibu litaleta desimali, basi hiyo desimali
unatakiwa kuachana nayo ili jibu libaki namba
nzima. Penye alama (x) hiyo ni ya kuzidisha.
Yafuatayo ni majibu niliyopata kwa hatua zote
baada ya kuuingiza mwaka 2017 ili kujua siku
ya Pasaka ya mwaka huu: (1): 3, (2): 20, (3):
17, (4): 5, (5): 0, (6): 4, (7): 1, (8): 1, (9): 6,
(10): 21, (11): 4, (12): 0, (13): 139, (14): 16,
(15): 4.
Tarehe imepatikana kwenye hatua ya 14
ambako jibu ni “16”. Mwezi umepatikana
kwenye hatua ya 15 ambako jibu ni “4”. Hivyo
Pasaka ya mwaka (2017) huu ni Tarehe 16,
mwezi wa 4.
Hivyo, kwa njia hii, unaweza kujua tarehe za
Pasaka kwa miaka ijayo kama unavyoijua
tarehe ya Krismas. Kama kuna tukio lilifanyika
siku ya Pasaka miaka iliyopita na hukumbuki
tarehe, basi tumia kanuni hii.
Zifuatazo ni siku zinazoitangulia Pasaka kwa
idadi ya siku zilizoandikwa kwenye mabano:
Jumatano Ya Majivu (46), Jumapili ya Matawi
(7), Ijumaa Kuu (2).
Zinazotanguliwa na Pasaka ni hizi zifuatazo:
Kupaa (42), Pentekoste (49), Utatu Mtakatifu
(56), Ekaristi (63).
Mwanzo tuliona kwamba Mwezi-Mkubwa wa
Pasaka au “Ecclesiastical full Moon” ni ule wa
March 22 hadi April 18. Ukitokea March 22
basi kuna uwezekano siku hiyohiyo ikawa
Pasaka na ikawa imevunja rekodi ya kuwahi
mapema.
Ukitokea April 18, kuna uwezekano wa Pasaka
kuwa siku saba zaidi ya hapa yaani April 25,
na hiyo ikawa ni tarehe ya juu mno ya Pasaka.
Hivyo, Pasaka yoyote haiwezi kuwa chini ya
Machi 22, wala haiwezi kuwazaidi ya April 25.
Pasaka tuliyoiona mwaka 2008 ndiyo ya
mwisho kwa kizazi chetu kuiona ikiwahi
mapema kiasi kile, kwani ilitokea Machi 23 na
itairudia tena tarehe hiyo mwaka 2160!
NB: iyo ni moja tu ya kanuni(formula) zitumikazo kupata tarehe na mwezi wa pasaka ya kila mwaka.
©Haki zote zimehifadhiwa
2017

Subscribe to:
Posts (Atom)
-
Kuna mafundisho mengi tofauti juu ya Mtu anapokufa, wengine wanasema anaenda kuzimu, wengine jehanamu, wengine peponi, wengine haendi ko...
-
UZINZI UPO HIVI...! 1.Humvunjia heshima mtu na anakuwa na jeraha moyoni. Kwa maana hiyo anakuwa mgonjwa kwa sababu anakuwa kaumia moyo. An...
-
Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wanaume wakisema wanawake wasomi na wenye vyeo ni "wasumbufu". Wengine wamefika mah...